Serikali imetoa Sh900 milioni kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa
kipindupindu nchini. Fedha hizo zilitolewa katika kipindi cha Novemba mwaka jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema watu 21,634
waliugua ugonjwa huo na wengine 338 kufariki dunia tangu ulipolipuka
Agosti 15 mwaka jana.
Kuongezeka kwa kasi ya kusambaa ugonjwa
huo nchini na ongezeko la wagonjwa na vifo kulimfanya Rais John Magufuli
kufuta sherehe za Uhuru (9 Desemba) na kuwataka wananchi wote akiwamo
yeye kushiriki usafi wa maeneo yao ya kuishi kuepuka ugonjwa wa
kipindupindu.
Alisema kuenea kwa ugonjwa huo nchini ni aibu kwa kuwa unatokana na uchafu ambao unaweza kusafishwa bila gharama yoyote.
Waziri
Ummy alizungumzia mgawanyo wa fedha hizo kuwa Sh520 milioni
ziligawanywa kwenye mikoa iliyoathirika na ugonjwa huo, Sh251.1 milioni
zilitumiwa kununulia dawa na vitenganishi.
Alisema Sh328.8
milioni zilitumika kwa kamati za afya kitaifa na pia kutekeleza shughuli
mbalimbali za uelimishaji jamii, mafunzo ya wataalamu wa afya na
kuwapeleka katika mikoa ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo.
Waziri
huyo alisema takwimu za mwezi uliopita zinaonyesha kuwa idadi ya
wagonjwa imepungua, sambamba na idadi ya mikoa na wilaya.
“Ifahamike kuwa maji na mazingira yetu bado yanaweza kutunza vimelea hawa wa kipindupindu na jitihada tulizojiwekea, nasisitiza ziwe endelevu kwa mikoa yote,” alisema Waziri Ummy. |
June 7, 2016
KIPINDUPINDU CHATAFUNA MILIONI 900
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment