Bunge
limetengua kanuni zake na kubadilisha muda wa kumaliza shughuli zake
kwa lengo la kuruhusu wabunge Waislamu kutimiza wajibu wao wa kiimani
katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Utenguzi
wa kanuni hizo ulipitishwa jana baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Bunge, Jenister Mhagama kuomba Kanuni ya 28(4),
ambayo kwa ujumla wake inaelekeza kwamba Bunge litaendelea kukaa hadi
saa 2:00 usiku.
Mhagama
aliomba kanuni hiyo itenguliwe na badala yake, kuanzia siku ya kwanza
ya Ramadhani, Bunge lirejee saa 10:00 alasiri kama ilivyo sasa na
kuahirishwa saa 12:00 jioni. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wote
waliokuwamo ndani.
|
June 7, 2016
MFUNGO WA RAMADHANI WAPANGUA RATIBA YA BUNGE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment