WANAFUNZI
wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Kampasi ya Arusha (kilichofutiwa
usajili), waliokuwa chini ya programu ya shahada ya miaka mitano ya
ualimu wa sayansi, wametakiwa kusoma ngazi ya cheti au stashahada.
Kama watataka kusoma ngazi ya juu, watapaswa kuomba upya udahili.
Aidha,
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imesema
wanafunzi waliokuwa wakipata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB), mikopo yao pia imesimamishwa.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Simon Msanjila alitoa agizo hilo jana kupitia taaarifa kwa
vyombo vya habari.
Profesa
Msanjila alisema hatua hiyo, inatokana na kubainika kwamba wanafunzi
hao hawastahili kusoma shahada na pia hawakustahili kupewa mkopo.
“Tunawafahamisha
wanafunzi wa SJUIT waliokuwa kwenye programu ya miaka mitano kwamba
watatakiwa kuishia daraja la cheti na stashahada... Kama wanafunzi hao
watataka kuendelea na masomo ya juu, watatakiwa kuomba upya,” ilisema taarifa hiyo.
Februari
25, mwaka huu, Wizara kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) baada ya
kujiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph
Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo
kikuu, ilifuta kibali cha kuanzishwa kwake.
Iliidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote, waliokuwa wanasoma katika Kampasi hiyo ya Arusha kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT.
Aidha, ilifuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi.
Ilielekeza
wanafunzi waliokuwa wakiendelea na masomo katika programu hiyo,
wahamishiwe katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam.
TCU
ilielekeza kwamba wanafunzi watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi
ya Stashada, kama ilivyokuwa imeidhinishwa na Tume hapo awali.
Wanafunzi waliohamishiwa kwenye vyuo mbalimbali, waendelee na masomo.
Taarifa
hiyo ilisema wakati wa mchakato wa uhamisho, wanafunzi wote
walihakikiwa kubaini kama wanakidhi vigezo vya kusoma kwenye ngazi
hiyo.
Wanafunzi wote waliokuwa wakisoma programu hiyo ya miaka mitano, walihamishiwa kwenye Kampasi ya Luguruni, jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kutokana na mchakato wa uhakiki, baadhi ya wanafunzi walikutwa hawana sifa za kujiunga na mafunzo hayo ya ualimu.
Wale
waliobainika kuwa na sifa, walitaarifiwa kuendelea na masomo kwenye
kampasi hiyo ya Luguruni.Wanafunzi katika kundi hili waliobainika kuwa
na vigezo, walitaarifiwa kuendelea na masomo katika Kampasi ya
Luguruni.
"Maana
ya kuwa na vigezo vya ufaulu tunavyovizungumzia hapa ni kwamba
wanafunzi husika wamefaulu katika masomo lengwa yanayowawezesha kusoma
Cheti cha Ualimu Daraja “A” ambacho ni kigezo cha kwanza kwa mujibu wa
mtaala wa programu hiyo."
|
June 7, 2016
MIKOPO YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST JOSEPH (SJUIT) YAFUTWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment