Udhaifu
wa Kanuni za Bunge katika kufafanua mambo mbalimbali ya uendeshaji wa
Bunge, umeelezwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwa unatakiwa
kurekebishwa ili kutoa nafasi ya Kiti cha Spika kutoa uamuzi dhidi ya
vitendo visivyokubalika vinavyoendelea ndani ya Bunge.
Amesema
hayo jana alipokuwa akitoa majibu wa muongozo alioombwa na Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe na Mbunge Nkasi Kaskazini, Ally
Keissy (CCM) kuhusu uhalali wa posho wanazolipwa wabunge wa Kambi ya
Upinzani, ambao wamekuwa wakiingia bungeni kusaini posho na kwenda
kupumzika.
Dk
Tulia alisema tangu Mei 30, mwaka huu, wabunge hao wamekuwa wakiingia
bungeni kusaini posho na kuondoka kwenda kupumzika, jambo
lililosababisha Dk Mwakyembe kuomba muongozo kama malipo hayo ni haki
kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya Katiba ya 23.
Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 23, ibara ndogo ya kwanza
na ya pili; “Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki
ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi
kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za
kazi wanayoifanya.Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya
haki.”
Akitoa
muongozo wake kama malipo hayo ya posho ni halali kwa mujibu wa Katiba
au la, Naibu Spika alisema ametumia uamuzi wa Kiti cha Spika uliotolewa
Aprili 27, 2016 kuhusu muongozo kama huo.
Alisema
Kiti cha Spika katika muongozo huo wa Bashe, kilinukuu Katiba Ibara ya
73 inayosema, “Wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa
mujibu wa Katiba hii, na watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa
mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.”
Mbali
na malipo hayo kulindwa na Katiba, Dk Tulia alisema pia Sheria ya
Uendeshaji wa Bunge Sura ya 15 na 19 Kanuni za Bunge zinaelezea kuwa
mbunge anapohudhuria vikao vya Bunge, atalipwa posho.
Dk
Tulia alisema vitendo vya kutohudhuria mjadala wa Bunge havikubaliki
kwa kuwa havikidhi matakwa ya Katiba Ibara ya 23, lakini akasema pamoja
na Kiti cha Spika kusisitiza kuwa kutohudhuria mjadala hakukubaliki,
lakini kuna haja ya kubadili sheria ili mbunge alipwe baada ya kumaliza
kazi.
Pia
alisisitiza kuwa Kanuni za Bunge zinazotumika katika kuwalipa posho,
hazijaeleza kwa uwazi maana ya neno mahudhurio, hivyo nazo zinahitaji
marekebisho kudhibiti hali hiyo.
Baaada
ya kutoa muongozo huo, Keissy alisimama na kuomba muongozo mwingine na
alipopewa nafasi, aliomba utaratibu wa kutumia mashine za kielektroniki
kusaini mahudhurio, ubadilishwe na badala yake urejeshwe ule wa zamani
wa mbunge kusaini katika karatasi.
Dk
Tulia akijibu muongozo huo, alisema hata ukirejeshwa utaratibu huo,
mbunge anaweza kusaini katika karatasi saa tano na kuondoka kwenda Dar
es Salaam na kusisitiza kunahitajika marekebisho ya Kanuni za Bunge ili
neno mahudhurio, lipewe ufafanuzi wa wazi.
Hata hivyo, aliahidi kuwasiliana na Katibu wa Bunge ili kuona utaratibu mzuri wa wabunge kusaini posho katika wakati wa sasa.
Baada
ya muongozo huo wa Naibu Spika, Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi maarufu Sugu alidai wao wataendelea kususia vikao vyote vya
Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika kwa madai kuwa anatumia Kanuni za
Bunge, kuwakandamiza.
Akiwasilisha
maoni ya kambi hiyo kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Udhibiti wa Matumizi
ya Dawa na Mbinu za Kuongeza Nguvu Michezoni, Mbilinyi alisema wabunge
wa Kambi ya Upinzani wanaposusa hawarudi nyumbani kupumzika, bali
wanashinda katika maktaba ya Bunge kufanya kazi.
Mbilinyi
alisema ni heri wabunge wa Kambi ya Upinzani wanaoshinda katika maktaba
ya Bunge, kuliko wa CCM wanaohudhuria vikao hivyo.
|
June 7, 2016
WABUNGE WA UPINZANI WANAOSUSIA VIKAO VYA BUNGE WATAENDELEA KULIPWA POSHO ZAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment