Washiriki
wa Shindano la kumsaka mlimbwende katika Manispaa ya Ilemela Mkoani
Mwanza la MISS ILEMELA 2016 (pichani), wakionyesha upendo wao kwa 102.5
Lake Fm Mwanza, walipotembelea Kituo cha Utamaduni Bujora kilichopo
katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza siku ya jana.
……………………………………………………………………………………………
Walimbwende
hao wamepiga kambi katika hotel ya “New Bujora Point” iliyopo Magu ili
kujinoa na fainali za shindano hilo linalotarajiwa kufanyika jumamosi
ijayo June 4, 2016 katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza,
ambapo kiingilio itakuwa shilingi 10,000 kawaida na shilingi 30,000 kwa
VIP huku wasanii mbalimbali wakiongozwa na Ney Wa Mitego wakitarajiwa
kudondosha burudani kali.
Pamoja
na mambo mengine, lengo la washiriki hao wa shindano la Miss Ilemela
2016 ambao mwaka huu ni 16, ni kutembelea kituo hicho ni kujifunza
masuala mbalimbali kuhusiana na utamaduni wa kabila la Kisukuma.
|
June 1, 2016
WASHIRIKI MISS ILEMELA 2016 WATEMBELEA KITUO CHA UTAMADUNI BUJORA KILICHOPO MAGU MKOANI MWANZA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment