Shirika
la Hifadhi ya Taifa ya Jamii NSSF Makao Makuu ikishirikiana na Ofisi ya
Mkoa wa Lindi Imechanga Jumla ya Shilingi Milioni 50 Kwa Ajili ya
Kuchangia Harambee ya Kusaidia Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi
Iliyoungua Moto Wiki iliyopita.
Kwa Kutambua Umuhimu wa Elimu kwa Watoto Shirika Hilo Kupitia
Mkurugenzi Mkuu Wake ,Aliewakilishwa na Meneja wa Mkoa Bi Nour Aziz
Limetoa ahadi hiyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Majaliwa Kasim Majaliwa Alieongoza Harambee Hiyo Ambayo Ilihudhuriwa na
Wadau Mbali mbali Akiwemo Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Mama Salma
Kikwete.
Katika Harambee Hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 80 Taslimu
zilichangwa Huku Ahadi na Vifaa vya Ujenzi zikifikia Shilingi Milioni
640 Ambapo Katika Ujenzi Mpya Waziri Mkuu Ameagiza Kujengwa Jengo la
Ghorofa litakalokuwa na Ofisi na Madarasa.
Katika Tukio Hilo la Moto,Jumla Ya Madarasa 9 na viti na Meza
zaidi ya 300,Ofisi 4 na Vyoo Matundu 24 Viliteketea na Moto Uliotokana
na hitilafu ya Umeme. (Picha na Abdulaziz Video, Lindi)
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa
Lindi, Bi Nour Aziz (kulia) akiwasilisha ahadi ya shirika hilo ya
kuchangia milion 50 katika harambee hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu,
Majaliwa Kassim Majaliwa, mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa
Lindi, Bi Nour Aziz akipeana mkono na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Mafao NSSF, Bw
Juma Namuna, baada ya shirika hilo kuahidi kuchangia Milioni 50.
Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Uhasibu NSSF mkoa wa Lindi, Jumbe Dona.
No comments:
Post a Comment