Aliyekuwa
mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo, Albert Msando amejiuzulu nafasi
yake hiyo kufuatia video chafu zilizomuhushisha kuvuja kwenye mitandao
ya kijamii hivyo ameamua kujiuzulu ili kuwajibika na kuomba radhi kwa
wananchi kwa kitendo hicho
Kiongozi
wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amethibitisha kupokea barua
hiyo na kukubaliana na kiongozi huyo kwa kitendo chake hicho cha
kuwajibika kisiasa huku akieleza kuwa, Bw. Msando amekuwa na mchango
mkubwa katika Chama chao.
"Nimepokea
barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya
Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo. Ndugu Msando anawajibika Kwani
anapaswa, nanukuu kutoka katika barua yake, "kuishi Kama mfano Kwa
jamii inayonizunguka".
"Ndugu
Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama
katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru
kwa moyo wake wa uzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini
yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri
atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama"- alisema Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wamsaidie katika jambo hilo analopitia saizi
"Nikiwa
Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika
kujisahihisha kwake. Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa
uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba" alimaliza Zitto Kabwe.
No comments:
Post a Comment