KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 19, 2018

JESHI LA MAGEREZA LAMJIBU SUGU

Jeshi la Magereza nchini limekanusha taarifa zilizoibuliwa na Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kuhusu kukosekana kwa sare za wafungwa zaidi ya 600, katika gereza la Ruanda alipokuwa amefungwa.

Msemaji wa Jeshi hilo Lucas Mboje, amesema kwamba sio kweli kwamba wafungwa hawana sare na hakuna kitu kama hiko, isipokuwa kuna mahabusu ambao wapo mule wakiendelea kusubiri kesi zao, na ndio huenda ambao aliwaona bila sare.

“Hiko kitu hakipo, halafu asichanganye mambo, kuna mahabusu ambao wao wanajulikana kwa mujibu wa sheria hawavai sare, sasa asichanganye, mtu akishafungwa inajulikana lazima avae sare, sasa kuna mahabusu pia, sio kweli kama kuna tatizo la sare hakuna mtu anakosa sare, hebu fikiria wafungwa karibia 600 kwenye gereza moja wakose sare ni kitu ambacho hakiwezekani, hiyo itakuwa ni issue nyingine”, amesema Lucas Mboje.

Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu) alipotoka jela kwa msamaha wa Rais alisema kwamba alilazimishwa kuvaa sare za jela wakati kuna watu amewakuta gerezani zaidi ya mia 6 wamekosa sare na wapo mule ndani.

No comments:

Post a Comment