February 11, 2015

BAADHI YA WAFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA MALAIKA KINONDONI


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia), akiongoza wafanyakazi wenzie kutoka kampuni hiyo pamoja na watoto kutoka kituo cha watoto yatima cha Malaika wakati baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam jana kuwasilisha kwa niaba ya wafanyakazi wenzao michango yao ya vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu.Mtoto Upendo (kulia) kutoka kituo cha watoto yatima cha Malaika akipokea sabuni za mche kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) wakati baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam jana kuwasilisha kwa niaba ya wafanyakazi wenzao michango yao ya vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu.Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (wanne toka kulia) akizungumza na Mwendeshaji Mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Malaika (wa tatu toka kulia) wakati baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walipotembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam jana kuwasilisha kwa niaba ya wafanyakazi wenzao michango yao ya vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu. Akishuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (wa tano toka kulia).

No comments:

Post a Comment