Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji
amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa namna yoyote katika uchaguzi
wa mwaka 2020.
Dk.
Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza kuwa kuna mambo
hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,
“Huu
ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya yaliyofanywa na Jecha? hii
inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe
umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya pili
kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme
kokote kule”alisema Mashinji.
Aidha,
akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji amesema kumekuwa na
ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio amekuwa kila
kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza mapambano na rushwa aliamini kwamba
angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti.
Hata
hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika mwaka mmoja wa Rais Magufuli,
amesema ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga marufuku
mikutano ya hadhara pamoja na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile
alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.
No comments:
Post a Comment