
Anuani ya Simu
“MKUUPOLISI”
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022)
2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022)
2135556
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
30 /11/2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA IRINGA AFARIKI DUNIA.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa
wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter
Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya
taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kakamba alizaliwa mwaka 1963
katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma
shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha
kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi
1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari
Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994
alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Marehemu alijiunga na Jeshi la
Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo
mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991),
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi ya nafasi alizowahi
kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa
Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi
katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na
mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa,
Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.Amen.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment