Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Dk. Luis Shika
ambaye mapema leo alitangazwa kununua nyumba mbili za Lugumi zilizokuwa
zikipigwa mnada na Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart).
Taarifa
iliyotokana na mnada huo mapema leo mchana zilieleza kuwa Dk Shika
amenunua nyumba hizo mbili zilizopo eneo la Mbweni, Dar es Salaam kwa
gharama ya Tsh 1.9 bilioni.
Taarifa
kutoka Yono zinaeleza kuwa, mnada wa nyumba hiyo unarudiwa tena leo
baada ya kubainika kuwa Dk Shika ni tapeli na kwamba ameshindwa kulipia
fedha asilimia 25 kama masharti ya mnada huo yanavyotaka.
Akiwajibu
waandishi wa habari maswali yao, Dk Shika alisema kwamba, Yono walitaka
25% ya fedha za nyumba hizo, ambapo yeye hakuwa na kiasi hicho cha
fedha kwa wakati huo.
Aidha,
alifafanua kwamba, kiasi hicho cha fedha kingeweza kupatikana kesho au
keshokutwa kwa sababu huwa hatembei na fedha kamili mfukoni.
No comments:
Post a Comment