Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka polisi wanawake kupambana na
vitendo vya kiuhalifu ikiwemo uchochezi, wizi wa mitandao, ujangili
ugaidi na utakatishaji wa fedha haramu.
Hayo ameyasema jana Novemba 9 akifunga maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao wa polisi wanawake yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha taaluma ya Polisi Kurasini.
Makamu wa Rais alisema suala la kuwepo kwa ulinzi ni muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.
Alisema
kwamba kuwepo kwa polisi wanawake kumeleta mtazamo tofauti katika
jamii, watu wamekuwa wakiona polisi ni rafiki wa umma.
Aliwataka polisi kufuata sheria katika matukio yote ya unyanyasaji wa kijinsia badala ya kuwaacha kwenda kuyatatua kifamilia.
" Unakuta mtu kanyanyaswa kijinsia anapofika kituoni polisi wanasema hiyo ni aibu mkayamalize kifamilia amesema Samia "
Katika
vita ya unyanyasaji wa kijinsia aliwataka polisi kushirikiana kutoa
elimu bila kujali jinsia kwani vita hiyo sio ya wanawake tu.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni aliwapongeza polisi kwa mshikamano pamoja na ujasiri waliouonyesha.
Masauni
aliwahakikishia polisi kuwa kila kitakachopatikana Serikalini
atahakikisha kinagawanywa kwa usawa ili kuhakikisha polisi wanafanya
kazi kwa ufanisi.
Naye
Kamanda wa Jeshi la Polisi mstaafu na mlezi wa mtandao huo Saidi Mwema
alisema alipokuwa mkuu wa jeshi hilo alipanga kubadilisha muundo wa
jeshi hilo.
Alisema
"nilipofanya ziara Afrika ya kusini na kuona muundo wao nilivutiwa nao
sana na niliporudi nchini nilianzisha mfumo huo"
Naye
mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Alvaro alisema katika
jeshi la Umoja wa Mataifa wapo pia polisi wanawake na wengine kutoka
Tanzania.
Hivyo nawapongeza kwa ujasiri na umoja wenu kwa kudhubutu ili kufikia malengo ya usawa wa kijinsia.
Katika
maadhimisho yalipambwa na vikosi mbalimbali vikiongozwa na polisi
wanawake ikiwemo gwaride, kuendesha pikipiki na farasi, kikosi vya
makomandoo pamoja na vyakutuliza ghasia.
No comments:
Post a Comment