Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkurugenzi
wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt Neema Rusibamayira amesema kuwa anafurahishwa na jitihada
zinazofanywa na taasisi zisizo za kiserikali kwa kuhakikisha
wanapambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Akizungumza
kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy mwalimu, Dkt Neema amesisitiza elimu juu ya masuala ya
afya kwa akina mama kuweza kupata elimu zaidi kwani wao ndo waathirika
wakuu wa ugonjwa wa kisukari.
Akitoa
rai hiyo baada ya matembezi hayo yaliyoanzia Muhimbili mpaka viwanja
vya Mnazi mmoja vikihusisha wadau mbalimbali, Dkt Neema amesema elimu
juu ya masuala ya magonjwa yasiyoambukizi yatasaidia kupunguza kwa
ongezeko la wagonjwa wa kisukari pia wananchi wawe na kawaida ya kupima
afya zao mara kwa mara.
Matembezi
hayo yameenda na kauli mbiu ya mwanamke na kisukari pia wadau walioweza
kushirikiana kwa pamoja ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
TANCDA, LIONS Club na TDA ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya
kisukari duniani yakienda na kauli mbiu ya mwanamke na kisukari.
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Benard Konga akizungumza baada ya
matembezi ya hisani ya kuhamasisha wananchi kupambana na magonjwa yasiyo
ya kuambukiza ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani
na mwaka huu yakienda na kauli mbiu ya Mwanamke na kisukari.
Mkurugenzi
wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt Neema Rusibamayira akizungumza baada ya matembezi ya hisani
ya kuhamasisha wananchi kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa
ni katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani na mwaka huu yakienda
na kauli mbiu ya Mwanamke na kisukari.
No comments:
Post a Comment