| Mwigamba akila kibano |
Na Elizabeth Hombo, Dar es Salaam
VURUGU zimetokea jana kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya makundi yanayopingana ndani ya Chama cha ACT-Tanzania kukutana ana kwa ana katika ofisi hiyo kwa ajili ya kikao cha usuluhishi.
Baada ya kukutana kwa makundi hayo, ghafla walitokea vijana wanaodaiwa kukodiwa na Mwenyekiti aliyesimamishwa, Kidawi Limbu na kumvamia Katibu Mkuu wa muda wa chama hicho, Samson Mwigamba. Vurugu hizo zimetokea ikiwa ni siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kumsimamisha uongozi Limbu na kumwondoa katika nafasi yake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kwa makosa ya kinidhamu.
Mwigamba alidai vijana hao wamekodiwa na Limbu kwa lengo la kumfanyia vurugu baada ya kuona mikakati yake imekwama ndani ya chama.

No comments:
Post a Comment