KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 30, 2015

PROF.JUMANNE MAGHEMBE: SERIKALI IMEVALIA NJUGA TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI NCHINI

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji  Mh. Prof. Jumanne Maghembe mara baada ya kuwasili katika kata ya Kileo jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro wakati alipoanza ziara ya kikazi ya jimboni humo akikagua na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa CCM. Akizungumzia tatizo la  maji nchini kwa ujumla Prof. Maghembe  amesema serikali iko katika utekelezaji wa miradi ya maji awamu ya pili ambapo serikali inatekeleza miradi  ya maji katika miji mikuu mbalimbali hapa nchini, ambapo ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa maji katika miji mbalimbali kufikia asilimia 75% wakati katika jiji la Dar es salaam upatikanaji wa maji utafikia asilimia 95, hata hivyo Prof. Maghembe amongeza kwamba miradi hiyo inatekelezwa kwa gharama kubwa na serikali ina nia ya dhati ya kumaliza tatizo hilo nchini kwa kiwango kikubwa. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANGA KILIMANJARO)
5
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Waziri Prof. Jumanne Maghembe wakishiriki ujenzi wa mifereji ya  skimu ya  umwagiliaji kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga.
11
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Waziri Prof. Jumanne Maghembe kushoto  wakipiga makofi kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mangara Lembeni wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
12
Waziri Prof. Jumanne Maghembe akicheza ngoma ya asili ya wapare huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma hiyo wakati alipowasili katika moja na vijiji alivyotembelea na kuzungumza na wananchi wilayani Mwanga.
13
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Waziri Prof. Jumanne Maghembe  wakishiriki ujenzi wa  jengo la KKKT  Mwaniko wilayani Mwanga
14
Waziri wa maji na Mbunge wa jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe  akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga 
18
Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga.
19
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo  uliofanyika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.                                       

No comments:

Post a Comment