Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hundi ya malipo ya Bima
ya Maisha(Flexi Provider) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la
Bima la Taifa(National Insurance Corporation of Tanzania Limited) NIC
Bwana Sam Kamanga ikulu jijini Dar es Salaam julai 21, 2015.
Akimkabidhi hundi hiyo, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Tanzania Limited (NIC) Bw. Sam
Kamanga amesema uwepo wa Mheshimiwa Rais kama mteja wa NIC imesaidia
kukuza uelewa na shughuli za shirika hilo.
“Kitendo cha Serikali kukatia Bima
mali zake na taasisi zake, kumeongeza uwezo wa kifedha wa shirika na
soko la Bima” amesema na kuwataka watu binafsi, taasisi mbalimbali na
mashirika ya kiserikali kukata Bima kwa ajili ya maendeleo na akiba ya
baadaye.
Rais Kikwete ameitaka NIC kuongeza
juhudi katika kuhamasisha na kuelimisha watanzania umuhimu na manufaa
makubwa yanayopatikana kutokana na Bima.
|
July 22, 2015
RAIS DKT KIKWETE APOKEA HUNDI YA BIMA YA MAISHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment