Tanzanite
inayowania kufuzu kwa Fainali za Kombe Duniwa mwaka 2016 nchini Papua New
Guinea, itacheza mchezo huo wa marudano siku ya jumamosi tarehe 25 Julai, jijini
Lusaka.
Katika
mchezo wa awali uliofanyika takribani wiki mbili zilizopita, Tanzanite
ilipoteza mchezo wake nyumbani baada ya kufungwa kwa mabao 4 – 0, hivyo
kuhitaji kushinda zaidi ya mabao 5 – 0 ili kuweza kusonga katika hatua
inayofuata.
Msafara
wa Tanzanite utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo
utajumuisha makocha Rogasian Kaijage (kocha mkuu), Edna Lema (kocha msaidizi),
Peter Manyika (kocha wa makipa), Christina Luambano (Daktari), Mwanahamis
Abdallah (mtunza vifaa) na Meneja Furaha Francis.
Wachezaji
watakaosafiri ni Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Donisia Minja, Najiat
Abbas, Neema Kiniga, Happyness Mwaipaja, Jane Lucas, Anastazia Katunzi, Anna
Mwaisura, Janet Pangamwene, Gelwa Rugomba, Blandina Ambros, Amina Ramadhan,
Asha Shaban, Maimuna Hamis, Zuwena Hamis, Amisa Athuman na Wema Richard.
VPL KUANZA SEPTEMBA 12
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) itaanza Sept 12 badala ya Agosti
22 ili kumpa Charles Mkwasa fursa ya kuendelea na program yake kuelekea mechi
ya Taifa Stars vs Nigeria itakayochezwa Sept 5.
Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayozikutanisha
Azam FC dhidi ya Yanga SC sasa itachezwa Agosti 22 badala ya Agosti 15.
Ratiba ya Ligi Kuu iliyokuwa imeandaliwa, sasa inafanyiwa
marekebisho kwa ajili ya tarehe mpya ya kuanza, ambapo pamoja na mambo mengine
mechi sasa zitachezwa wikiendi na katikati ya wiki na wikiendi ya Oct 25
hakutakuwa na mechi kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Klabu za Ligi Kuu zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe mpya ya
kuanza Ligi, na dirisha la usajili linabaki kama lilivyo.
Wamiliki wa viwanja vyenye upungufu wmeandikiwa barua kutakiwa
kurekebisha upungufu katika muda maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa kutumika
kwa ajili ya PL na FDL.
Timu ya Madini ya Arusha imeruhusiwa kutumia Uwanja wa Nyerere
uliopo Mbulu mkoani Manyara kwa mechi za SDL kwa masharti upungufu uliopo
kwenye uwanja huo urekebishwe kwanza.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment