Mkurugenzi Mkuu Mpya – TCRA, Dk. Ally Y. Simba |
……………………………………………………….
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa hivi karibuni alimteua Dk. Ally Yahaya Simba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA) kufuatia mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 kifungu cha 9 na kifungu cha 13. (TCRA Act, 2003)
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa hivi karibuni alimteua Dk. Ally Yahaya Simba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA) kufuatia mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 kifungu cha 9 na kifungu cha 13. (TCRA Act, 2003)
Dk. Simba aliteuliwa rasmi kushika
wadhifa huo mnamo tarehe 6 Jula1 2015 kwa kipindi cha miaka mitano.
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Simba alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia tangu Agosti 2013. Dk. Simba ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16
katika Sekta ya Mawasiliano ambapo amefanya kazi kwa watoa huduma,
Taaluma ya Utafiti, Udhibiti pamoja na Serikali Kuu.
Dk. Simba ana Shahada ya B.Sc. (Hons.) Shahada ya Sayansi ya
Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Tanzania, aliyopata mwaka 1998. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Uhandisi
aliyoipata mwaka 2003 na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) ya Uhandisi wa
Kielektroniki kutoka Chuo Kikuu Cha Hokkaido, Sapporo, nchini Japan,
aliyoipata mwaka 2006. Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2011, Alikuwa Mtaalamu
Mtafiti katika Taasisi ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
huko Tokyo, Japan, ambako alihusika katika kufanya utafiti wa madhara ya
ya kiafya kwa mwanadamu kwa kutumia simu za mikononi na kwa kuwa karibu
na minara ya mawasiliano.
Mnamo mwaka 2011 hadi mwaka 2013, alifanya kazi Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama Meneja Mipango na Utafiti wa Mamlaka.
Dk. Simba ametoa machapisho kadhaa yaliyosambazwa kote duniani
katika majarida ya kimataifa na amewasilisha matokeo ya tafiti zake
katika zaidi ya mikutano 30 ya kimataifa ndani na nje ya Tanzania. Aidha
Dk. Simba alikuwa Kiongozi wa timu ya wataalamu wa Kitanzania
iliyoandaa Sheria za Uhalifu wa Mitandao nchini iliyopitishwa na Bunge
hivi karibuni.
Dk. Simba ni Mhandishi Mahiri
(Chartered Engineer), aliyesajiliwa nchini Uingereza katika Baraza la
Uhandisi nchini humo na ni “Fellow” wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia
ya nchini Uingereza, ambako alifanya kazi kama Mshauri wa Kimataifa wa
Usajili wa Wanataaluma Wahandisi kutoka Aprili 2011 mpaka Machi 2014.
Pia Dk. Simba ni Mwanachama wa “Institute of Electrical and Electronics
Engineers” (IEEE). Hali kadhalika Dk. Simba amechapishwa katika jarida
la “Marquis Who’s Who in Science and Engineering” katika toleo la 11, la
mwaka 2011–2012.
Dr. Simba ni miongoni waliopata Udhamini wa Serikali ya Japan (Monbusho Scholarship) kutoka mwaka 2000 mpaka 2006.
No comments:
Post a Comment