KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 20, 2015

THE STARS BAND YAZINDULIWA DAR

DSC_0035 (2)
Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Aneth Kushaba imezinduliwa rasmi siku Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikisindikizwa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano akionesha mambo yake kwenye stage hii yote ni wakati anajitambulisha kwa mashabiki wa bendi waliofika kwenye uzinduzi wa bandi hiyo.
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Seghito mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangozi akijitambulisha kwa kuonesha uwezo wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika katika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar.
Mpiga la Gitaa katika Bendi ya The Stars, Othuman Majuto akionesha ujuzi wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo.                    

No comments:

Post a Comment