KWAMBA TAREHE 01.06.2016 MAJIRA
YA SAA 12:30HRS KATIKA MAENEO YA KABANGAJA – MNARANI KATA YA BUGOGWA
WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA ASKARI WALIOKUWA DORIA PAMOJA NA MISAKO
YA WAHALIFU NA UHALIFU WALIMKAMATA LETICIA ELIAS MIAKA 52 MKAZI WA
IGOMBE AKIWA NA MISOKOTO 12 YA BHANGI PAMOJA NA MWENZAKE AITWAYE THOMAS
LIPOVITIA MIAKA 49 MKAZI WA KIBAGAJA AKIWA NA KILO 02 ZA BHANGI KITENDO
AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA BAADA YA ASKARI KUWAKAMATA
WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU WALIENDELEA NA MSAKO WA KUSAKA WAHALIFU
WENGINE NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MAJANI MANYEGO MIAKA 38 AKIWA NA POMBE
AINA YA GONGO LITA 10 KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.
WATUHUMIWA WOTE WATATU WAMEKAMATWA WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA
POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU
ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO YANAHARIBU NGUVU KAZI YA TAIFA LETU, HIVYO
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LITAWASAKA KILA SEHEMU WAHALIFU WA AINA
KAMA HIYO NA KUHAKIKISHA WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA
SHERIA.
IMESAINIWA NA
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
|
June 2, 2016
TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MWANZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment