February 11, 2015

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KITUO CHA AFYA MBAGALA

 Mratibu wa Takwimu wa Manispaa ya Temeke, aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk. Samuel Lema (wa pili kulia) akimshukuru Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Alen Mwebuga (kushoto), baada ya kukabidhiwa jana kisima kipya kilichojengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil 24 katika Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table Dar es Salaama. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Batuli Luhanda.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table,Dk. Batuli Luhanda akimshukuru Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Alen Mwebuga (kushoto), baada ya kituo hicho kukabidhiwa jana kisima kipya kilichojengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil 24.Kulia kwake ni Mratibu wa Takwimu wa Manispaa ya Temeke, aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk. Samuel Lema.
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya kampuni hiyo ya kuboresha sekta ya maji katika baadhi ya hospitali, Vituo vya Afya na zahanati nchini, Kulia ni Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Alen Mwebuga.

No comments:

Post a Comment