Na Anna Nkinda – Nairobi, Kenya
…………………………………..
Asillimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika
nchi zinazoendelea na katika Bara la Afrika lenye watu zaidi ya milioni
804 asilimia 12.4 wanapata saratani kabla ya kufikia umri wa miaka 75
na asilimia 90 wanapata ugonjwa huo wakiwa na umri wa chini ya miaka
40.
Hayo yamesemwa na Rais wa Kenya
Mhe. Uhuru Kenyatta wakati akifungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake
wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi
ambazo ni mlango wa kizazi, matiti na tezi dume unaofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta (KICC) uliopo mjini Nairobi.
Rais Kenyatta alisema Ripoti ya
saratani iliyotolewa mwaka 2014 na Shirika la Kimataifa la kutafiti
saratani kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ilionyesha
takwimu mpya za saratani zinaongezeka kila mwaka na kwa upande wa
Afrika vifo vingi vinatokana na saratani ya mlango wa kizazi.
“Watu wanapoteza maisha na kuugua
saratani kutokana na kutokuwa na uelewa wa ugonjwa huo, kutokuchukua
hatua za mapema na watu kutambulika kuwa na ugonjwa wa saratani wakati
umefikia hatua ya mwisho kutokana na hili tutaendelea kuwa na wagonjwa
ambao wanapata maumivu, wanashindwa kupata matibabu kwa wakati na
uangalizi wa karibu katika bara letu”.
Ni lazima tuhakikishe jamii
inajulishwa kuhusu ugonjwa wa saratani na kubadilisha aina ya maisha
tunayoishi kama watu wataacha kuvuta sigara, watakula vyakula vyenye
afya, atapunguza kunywa pombe na kufanya mazoezi mara kwa mara tutakuwa
tumezuia asilimia 40 ya saratani”, alisema.
Aidha Mhe. Rais Kenyatta alisema
katika bara la Afrika ugonjwa wa saratani siyo moja ya agenda inayopewa
kipaumbele katika masuala ya afya ukilinganisha na magonjwa mengine kama
ya kuambukiza lakini sasa ili kupambana na saratani kunatakiwa kuwa
na mikakati kwa nchi chache ambazo zitaweza kukutana na kufanya utafiti
na kutoa matibabu ili kuzuia watu wasife na hivyo kuokoa maisha katika
hatua ya mwanzo ya ugonjwa.
Mhe.
Rais Kenyatta alimalizia kwa
kusisitiza kuwa watu wanahitaji kupata chanjo ya hepatitis ambayo
inazuia saratani ya Ini na Human Papilloma Virus (HPV) inayozuia
saratani ya mlango wa kizazi ambazo zitasaidia kupunguza idadi ya
saratani katika bara la Afrika.
Akiwakaribisha wake wa marais na wadau mbalimbali wa afya waliohudhuria mkutano huo Mke wa Rais wa Kenya Mhe. Mama Margaret
Kenyatta alisema ni muhimu wadau hao wakaendelea kushirikiana na kufanya
kazi kwa pamoja ili kukabiliana na magonjwa hayo ya saratani.
Mhe. Mama Kenyata ambaye ni
Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza
magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni mlango wa kizazi,
matiti na tezi dume kwa mwaka 2015 – 16
Alisema wamefanikiwa kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa ya saratani wanachotakiwa kukifanya hivi sasa ni kuendelea kuhamasisha jamii ili waweze kujichunguza dalili za awali za saratani na kutibiwa kuzuia kwani saratani nyingi zikigundulika mapema zinatibika.
Alisema wamefanikiwa kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa ya saratani wanachotakiwa kukifanya hivi sasa ni kuendelea kuhamasisha jamii ili waweze kujichunguza dalili za awali za saratani na kutibiwa kuzuia kwani saratani nyingi zikigundulika mapema zinatibika.
“Tunatakiwa
kuwashawishi viongozi, Serikali na sekta binafsi na taasisi zisizo za
kiserikali kuchukua hatua za lazima ili kuweza kukabiliana na saratani
na hivyo kuokoa maisha ya watu wetu”.
Kuhusu ulaji wa vyakula alihimiza
ni muhimu waafrika wakaangalia maisha ya zamani na kurudi nyuma kwa
kuanza kula vyakula vya asili na kuacha kula vyakula vilivyosindikwa
hasa kwa vijana”
Mkutano huo wa siku tatu wenye
kauli mbiu ya wekeza kuokoa maisha: wajibu wa ushirikiano wa sekta
binafsi ulihuhuriwa na wake wa Marais kutoka nchi 12 akiwemo Mke wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Salma Kikwete.
No comments:
Post a Comment