Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akielekea kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyetta huko
Nairobi kuhudhuria mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Nchi za Afrika
unaozungumzia magonjwa ya saratani ya matiti, shingo ya kizazi na tezi
dume tarehe 20.7.2015.
PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na
Mke wa Rais wa Niger Madame Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakiwa
kwenye sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa nchi za
Afrika. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru
Kenyetta (hayupo pichani) tarehe 20.7.2015.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na
wake wa Marais kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamesimama wakati
wimbo wa Taifa wa Kenya ukiimbwa.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwa amesimama na baadhi ya
wake wa Marais wa Afrika wakati wimbo wa Mataifa ya Afrika ukiimbwa.
Kushoto kwa Rais Kenyatta ni Mkewe Mama Margret Kenyatta akifuatiwa na
Mke wa Rais wa Namibia Mama Monica Geingos, Mama Salma Kikwete na mwisho
ni Mama Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wa Niger.
Baadhi ya Wake wa Marais wa Nchi
za Afrika wakishiriki kumvisha mkanda maalum kwa kuteuliwa kwake kuwa
Balozi wa Hiari kwenye Masuala ya Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika.
Wanaomvisha mkanda huo kwa niaba ya wake wa Marais ni (kutoka kushoto
kwenda kulia) Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa
‘Forum of African First Ladies against Cervical, Breast and Prostate
Cancer, Mama Dkt. Lalla Mahammadou wa Niger, Mama Monica Geingos wa
Namibia, Mama Mary Ayen Mayardit wa Sudan Kusini. Mama Salma Kikwete na
Mwisho ni Mama Mathato Mosisili wa Lesotho.
No comments:
Post a Comment