Coastal Union |
KLABU
ya Coastal Union imeweza kusajili wachezaji 13 ambao wataitumikia timu hiyo
katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao Tanzania bara unaotarajiwa kuanza
kutimua vumbi Septemba mwaka huu hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa wametoka timu mbalimbali hapa nchini na nje
ya nchi.
Aliwataja
wachezaji hao kuwa ni Abasalim Chidebele ambaye ni mshambuliaji kutoka timu ya
Stand United, Kiungo Mkabaji Adeyum Salehe kutoka JKU ya Zanzibar,Kiungo
Mshambuliaji Nasoro Kapama kutoka Ndanda FC ya Mtwara,Beki wa kati Ernest
Mwalupani kutoka Ndanda FC ya Mtwara.
Wengine
ni Beki wa Kushoto ,Yassin Mustapa Salim kutoka Stand United,Kiungo Sultan Juma
kutoka klabu ya African Sports,Mshambuliaji Ahmde Shiboli kutoka Klabu ya
African Sports,Mohamed Hamis Mititi ambaye ni mchezaji huru.
Assenga
amewataja wachezaji wengine kuwa ni Benedict Haule ambaye alisajiliwa akiwa
kama mchezaji huru ambaye ni mlinda mlango,Mshambuliaji Ismail Mohamed Suma kutoka Stand United, winga wa
kushoto ambaye ni mchezaji huyo Patrick Protas Kamuhagile.
Amesema
wachezaji wengine ni Jackson Sabweto ambaye ni Mlinda Mlango kutoka Klabu ya
VILLA FC ya nchini Uganda amesaini mkataba wa miaka miwili,Yossouph Sabo kutoka
Klabu ya Younde FC ya Cameroon ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Wachezaji
wa zamani waliobaki kutimukia klabu hiyo kuwa ni Bakari Mbwana “Kibacha”,Abdallah
Mfuko,Hamadi Juma,Ibrahim Chuma,Ike Bright Obina,Abdulhalim Humud,Godfrey Wambura,Ayoub
Semtawa na Sued Tumba.
Wakati
huo huo wachezaji uongozi wa Coastal Union umewapandisha wachezaji watano
kutoka timu ya vijana ya Coastal Union kutokana na uwezo wao kuwa mzuri na wa
kuridhisha.
Waliopandishwa
ni Mohamed Shekuwe,Sabri Sabri,Tumaini Bakari,Fikirini Suleiman na mtenje
Albano.
No comments:
Post a Comment