Majambazi watatu waliuawa wakati wakirushiana risasi na polisi eneo la Tuangoma, Kigamboni huku wengine wawili wametiwa mbaroni .Kamnada wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam Suleiman Kova alisema majambazi hayo yalitiwa mbaroni tarehe 17 mwezi huu kufuatia uvamizi yalioufanya kituo cha Polisi Stakishari Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuua polisi na raia.Alisema fedha na silaha yalikuwa yamezichimbia chini ya ardhi na kuweka kinyesi juu.Majambazi yaliyokamatwa yalipobanwa yalikwenda kuonyesha silaha yalipoficha na ndipo zikakamatwa bunduki 15 na Shilingi milioni 170. |
Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na Waandishi wa Habari kuwaleza jinsi majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Stakishari yavilivyokamatwa na mengine kuuawa. |
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akiwaonyesha Waandishi wa Habari silaha zilizoporwa na majambazi kituo cha Polisi Stakishari hivi karibuni . |
Maburungutu ya fedha za majambazi hao yakionyeshwa kwa Waandishi wa Habari. |
Kamada Kova akiwaonyesha Waandishi wa Habari, picha za Majambazi yanaotafutwa na Polisi |
Pikipiki zilizokuwa zinatumiwa na majambazi waliovamia kituo cha polisi cha Stakishari Ukonga Jijini Dar es Salaam,zikiwa mbele ya Kamanda Kova. |
No comments:
Post a Comment