Kamishna
wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA akiwaonyesha wanahabari
silaha bunduki 16 zilizokutwa zimefukiwa chini huko pwani mkuranga huku bunduki
14 zikiwa ni zile zilizoporwa katika shambulio la kuvamiwa kituo cha polisi
stakishari jijini Dar es salaam.
Jeshi la polisi nchini Tanzania leo
limetangaza kupata mafanikio makubwa katika operation maalum inayoendelea ya
kuwasaka watu waliohusika katika shambulio la kuvamia kituo cha polisi cha
stakshari jijini Dar es salaam na kuendesha mauaji ya askari wanne wa kituo
hicho pamoja na raia waliokua katika kituo hicho huku wakipora kiasi kun]kubwa
cha silaha na kutokomea kusikojulikana.
|
Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dare s salaam
kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA amesema kuwa
jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wema wamefanukiwa kukamata bunduki
16 huku 14 zikiwa ni zile zilizoibiwa katika tukio la kituo cha staki shari na
mbili zikiwa bado hazijulikani ziliporwa kwa watu gani.
Amesema kuwa zoezi la kuwasaka watuhumiwa hao
lilianza mara baada ya kutokea kwa tukio la stakishari ambapo ilipofika tarehe
17 mwezi huu majambazi hao walijipanga kufanya tukio myinginme maeneo ya
mbagala jijini Dar es salaam ambapo wananchi walitoa taarifa kwa jeshi la
polisi na wakajipanga tayari kuwakabili.
|
Hili
ndio sanduku lililokua limehifadhi pesa taslimu million 170 na kufukiwa chini
huko mkuranga
Amesema kuwa baada ya kufika eneo la Twangoma mbagala polisi
walijipanga kuwakabili na baadae majambazi hao walitokea na kuanza
kushambuliana na askari hao ambapo katika mapamano hayo majambazi watano
walikamatwa ambapo watatu kati yao walikuwa tayari wameshakufa na wawili wapo
hai hadi leo.
Katika taarifa nyingine ambazo jeshi la polisi
kanda maalum ya dare s salaam walizipata jana tarehe 19 ni kuwa kulikuwa na
taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna tetesi kuwa silaha zilizoibiwa kituo cha
stakishari zilikuwa zimefichwa katika maeneo ya Tuangoma, Kigamboni.
|
Jeshi la polisi waliweka
kambi katika maeneo hayo na kuanza msako maalum wa kuzisaka mahali ambapo
silaha hizo zilikuwa zimefichwa ambapo katika tukio la kushangaza lilionekana
eneo ambalo lilikuwa limewekwa kinyesi cha binadamu na polisi kupatilia mashaka
na ndipo walipoamua kupachimba na kufanikiwa kupata silaha hizo.
Baada ya
kuchimba maeneo hayo jeshi la polisi lilifanikiwa kukuta silaha aina mbalimbali ambazo ni
bunduku aina ya 16 ambazo 14 ni za stakishari,na risasi 55 huku risasi 28 ni
zile zilizoibiwa katika tukio la stakishari.
Pamoja na silaha hizo jeshi hilo
lilikuta sanduku kubwa lililokuwa na hela kiasi cha shilingi million sabini
ambazo hazikujulikana mara moja zilikuwa na lengo gani huku KOVA akisema kuwa
uchunguzi zaidi unaendelea.
Aidha kamishna kova amesema kuwa pamoja na
mafanikio hayo yaliyopatikana katika operation hiyo bado jeshi la polisi kanda
maalum ya Dar es salaam linaendelea na kazi kubwa ya kuwasaka wahalifu hao kwa
kuwa bado kuna silaha nyingi ambazo ziliporwa katika tukio la stakishari na
bado hazijapatikana.
TAARIFA ZAIDI NTAZIDI KUKUPA BAADAE
|
No comments:
Post a Comment