Hissène Habré azungukwa na askari baada ya kusikilizwa na jaji tarehe 2 Julai mwaka 2013 katika mji wa Daka
Na RFI
Pazia
inafunguliwa leo Jumatatu asubuhi katika mji mkuu wa Senegal, Dakar
katika kesi muhimu barani Afrika ya rais wa zamani wa Chad, Hissène
Habré.
Rais huyo
wa zamani wa Chad, alikimbilia nchini Senegal tangu kuangushwa
madarakani mwaka 1990, na anatuhumiwa makosa ya uhalifu dhidi ya
binadamu, uhalifu wa kivita na mateso.
Itakua
mara ya kwanza katika historia rais wa zamani kuhukumiwa katika nchi
ambayo si yake kwa uhalifu unaohusiana na haki za binadamu.
Hakuna
mtu angeliweza kufikiria kwamba siku moja Hissène Habré atafikishwa
mbele ya vyombo vya sheria ili kujibu matendo yake. Ili kigogo huyo wa
zamani wa Chad aliye jihusisha na mabaya mengi nchini aweze kufikishwa
mbele ya vyombo vya sheria, ilichukua zaidi ya miaka 15 ya vita kali vya
kisheria, vilioendeshwa na waathirika wakiongozana na mashirika
mbalimbali ya haki za binadamu, kwa njia ya kupambana dhidi ya ukatili,
maamuzi kuahirishwa, hukumu juu ya rufaa,... hadi hatimaye Senegal, kwa
makubaliano na Umoja wa Afrika, kuamua kuanzisha Kitengo cha Mahakama ya
Afrika kilichozinduliwa mwezi Februari mwaka 2013.(P.T)
Kesi ya
rais wa zamani wa Chad Hissène Habré iliyokua ikisubiriwa kwa muda mrefu
itaendeshwa katika Mahakama kuu Lat Dior, mjini Dakar kuanzia Julai 20,
2015.
" Leo hii
ni ushindi wa mshikamano, uvumilivu na mawazo. Mtu mmoja kwa waathirika
wa serikali hii ya kikatili ", amesema mwanaharakati mmoja wa haki za
binadamu, Reed Brody, huku akibaini kwamba " Jambo ambalo lilikua
halifikiriwi miaka iliyopita, sasa linawezekana na hii inafungua njia
kwa waathirika wengine barani Afrika na ulimwenguni ".
Uchunguzi
ulidumu miezi 19. Majaji waliunda tume nne na kujielekeza nchini Chad,
mashahidi na waathirika 2,500 walihojiwa na hasa kuzifanyia kazi nyaraka
za za zamani za DDS, ambayo iklikua polisi wa kisiasa wa Hissène Habré.
Rais wa zamani akataa kusikilizwa na mahakama
Kwa
upande wake, rais wa zamani wa Chad haitambui mahakama ambayo
itamsikiliza na kumuhukumu. Hissène Habré alikua akikaa kimya wakati wa
kusikilizwa, na amesema kupitia wanasheria wake kuwa amekataa kuhudhuria
vikao mahakamani. "Kesi hii ni kama mchezo wa kuigiza, na ntakubali
kusikilizwa iwapo wataamua kubadili mkakati, Hissène Habré hataki
kuhudhuria vikao", wamearifu wanasheria wa rais wa zamani wa Chad.
Katika hali yoyote, atakaa kimya. " Habré anakataa kujidhalilisha mbele
ya mahakama hiyo asiyoitambua", amesema mmoja wa watetezi wake, ambaye
ameshutumu kuwa " kesi ilipangwa tangu kitambo baada ya uchunguzi na
Habré alituhumiwa makosa kadhaa", " hii ni dhulma dhidi ya mteja wetu",
amesema mwanasheria huyo wa Hissène Habré.
Kesi hii itadumu miezi mitatu
Kulingana
na sheria za Senegal, Jaji mkuu ana uwezo wa kumfikisha mahakamani kwa
nguvu rais wa zamani wa Chad, hadi kufungwa pingu kama atakataa kuripoti
mahakamani. Je Jaji huyu mkuu atalazimika kutumia sheria hiyo? Mpaka
sasa haijajulikana kwa siku ya leo ufunguzi wa kesi ya rais huyo wa
zamani wa Chad.
|
No comments:
Post a Comment