![]() |
Machali ataambatana na Madiwani
wawili,Kamishna wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na
makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini.,
Pia katika
mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea na
makatibu uenezi 9 wa jimbo la Kasulu mjini yenye jumla ya kata 15 za
uchaguzi Mbali na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali
kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo siku ya jumanne julai 21/2015 ni
pamoja na wenyeviti wa matawi 101 na makatibu 98, watakaoambatana na
wanachama wa awali 648.
Wanachama na viongozi wote hao wanatoka katika
Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini.
Baada ya Mapokezi hayo ya
wanachama wapya wa ACTWazalendo, Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe ataelekea
mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapokea viongozi na madiwani kutoka
vyama mbali mbali zoezi litakalofanyika siku ya jumamosi julai 25.
Julai 26 Kiongozi wa Chama atakutana na watia azma wa nafasi ya Ubunge katika majimbo ya jiji la Dar esSalaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi Wakati kiongozi wa Chama akiwa mikoani kwa ajili ya kuwapokea wanachama wapya, jijini Dar esSalaam siku ya jumatano julai 22 viongozi wengine watakuwa na jukumu la kuwapokea wanachama na waliokuwa madiwani katika vvama tofauti.
Abdallah Khamis Afisa Habari -ACT-Wazalendo. 0777 008686 Imetolewa leo julai 20/2015
No comments:
Post a Comment