Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akikagua ujenzi wa Bara bara ya Wete hado Konde ambao uko katika hatua ya lami alipokuwa Kisiwani Pemba kwa ziara ya siku tatu kuagua shughuli mbali mbali za Maendeleo. Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Kamati ya Msikiti wa Ijumaa wa Micheweni Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwakumbusha waumini wa dini ya kiislamu kuendelea na ibada zao wakiepuka fitna za kuchanganya na siasa. Picha na Hassan Issa wa - OMPR - ZNZ.
Harakati za ujenzi wa Bara bara ya Wete hadi konde ikiwa miongoni mwa mradi wa Bara bara tatu Kisiwani Pemba zinaendelea baada ya maridhiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mjenzi wa mradi huo Kampuni ya Mwananchi Contracting Company Engineering { MECCO }.
Ujenzi wa Bara bara hizo wa awamu ya kwanza wenye urefu wa Kilomita zaidi ya 30 ulioanza rasmi Tarehe 15 Mei mwaka 2009 umekuwa ukisua sua kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo uchelewaji wa feha kutoka kwa mfadhili wa mradi huo Benki ya Maendeleo ya Kiislamu(BADEA)
No comments:
Post a Comment