KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 24, 2016

MFAHAMU KOFFI OLOMIDE, ANA UTAJIRI WA SH.BILIONI 40 ZA KITANZANIA

https://mpasho.co.ke/wp-content/uploads/2015/03/KOFFI-OLOMIDE-5.jpgMwanamuziki wa Kongo  Koffi Olomide  ambaye anajulikana kwa ngoma zake kali ana utajiri wa dola za Kimarekani milioni 18 karibu Shiliongi bilioni 40 za Kitanzania kwa mujibu wa utafiti wa mwaka huu .

 Majina halisi ya Koffi ambaye pia ni muasisi la Quartier Latin International orchestra ni Antoine Christophe Agbepa Mumba alizaliwa mwaka Julai 13, 1956, mjini  Kisangani nchini  Kongo. Akiwa kijana  alipenda kuimba na kupiga kitaa.
Alipata nafasi ya kwenda kusoma nchini Ufaransa,vyanzo vinasema kwamba ana Shahada ya pili katika Hisabati,nyingine ni Shahada ya kwanza katika Uchumi, Shahada zote hizo alizisomea nchini Ufaransa
  Alirudi Kongo miaka ya sabini na kujiunga na kundi la  Viva la Musica chini ya Marehemu Papa Wemba akiwa mtunzi na mwandishi wa nyimbo.

Koffi alianzisha kundi lake la Quartier Latin mwaka 1986 ana kufanikiwa kupata wapenzi wengi Afrika na Ulaya .
 Ana tuzo mbalimbali kama vile Mwanamuziki Bora wa Afrika, na nyingine za Kora .Chanzo Mtandao wa Net Worth

No comments:

Post a Comment