KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 24, 2014

DAKTARI ALIYEKUTWA AMELEWA AVULIWA CHEO GEITA

Wagonjwa wakimtia adabu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Nyakabale mkoani Geita, Josephat Msafiri baada ya kuwatelekeza juzi. Picha Jackline Masinde
 Geita. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Magreth Nakainga amemvua madaraka Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyakabale, Josephat Msafiri kwa kukiuka miiko ya kazi yake na kulewa wakati wa kazi.Mkurugenzi huyo aliamua kuchukua uamuzi huo jana kutokana na tukio lililotokea Juzi hii la daktari huyo kufunga kituo cha afya na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa, kisha kwenda kunywa pombe jambo lililowalazim wagonjwa  kumchapa viboko akiwa baa.“Tumeshamchukulia hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka yake ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa Serikali,” alisema Nakainga.Alisema kitendo alichokifanya kimeidhalilisha taaluma ya afya na madaktari kwa ujumla.Alisema tabia kama hizo hazitavumilika kwa mtumishi yeyote atakayekiuka maadili ya kazi.Pia alisema amepeleka wahudumu wa afya wakiwamo wauguzi wawili na daktari mmoja katika zahanati hiyo na huduma zinaendelea vizuri.Alipopigiwa simu jana ili azungumzie uamuzi huo, daktari huyo alianza kumlaumu mwandishi aliyeandika habari ya tukio hilo akisema kuwa amemharibia kazi.“Sikutegemea kama wewe uko hivyo, sasa nimekujua kumbe uko hivyo, Mungu mkubwa, yaani mmepigiwa simu na watu na kuamua kuja kuniharibia,” alisema Dk Msafiri na kukata simu kisha akaandika ujumbe uliosema: “Sikukujua sasa nimekujua vizuri, Mungu mkubwa. “

No comments:

Post a Comment