Imeandikwa na Samson Chaz
Mchana wa leo(jana) watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi waliovamia na kupora
ktk duka la Pesa Morocco, Kinondoni - hapa Dar, wamempiga risasi dada
Glory Rocky ambaye taarifa nazozipata ni kuwa dada huyu amepoteza
maisha Muhimbili National Hospital wakati anatibiwa. nimejaribu
kumtafiti na kukuta picha hii ambayo alipiga na mumewe mpendwa
Rwegoshora Makaka kwa kweli siwafahamu, ILA MUNGU AWATIE NGUVU Familia
nzima katika kipindi hiki cha sikukuu ambacho kimegeuka kuwa janga kubwa
kuwahi kuwakumba. - Majambazi walivamia kiduka cha M-PESA, tiGO PESA na
Airtel Money; wakati wanaondoka wakawa wanapiga risasi ikampata huyu
dada.aliyekuwa anapita barabarani hajui hili wala lile. Hatujui siku wala
saa manake sio kazi Glory aliwaaga rafiki zake kuwa wataonana lakini
ndo haya tena.KWA HISANI YA TANZANIA CLASSIC
No comments:
Post a Comment