MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za
kibongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, leo ametoa msaada wa vitu mbalimbali
katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi
Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mrembo huyo ambaye pia ni
mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti inayojihusisha na masuala ya urembo,
alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya
kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na
wengineo wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi
msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa
hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.
“Nimefika
hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya
watoto kama hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao
kujiona ni sehemu ya jamii ya Watanzania,” alisema.
Kidoti alitumia
fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi
mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii
kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.
Msaada
aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga
wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne,
alitoa pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo
kusaidia makundi maalum.
Akielezea changamoto zilizopo katika kituo
hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto
wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za matibabu pamoja na
kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji.Miss
Tanzania namba mbili 2006, Mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate
Mwegelo, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima
cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa
zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele,
unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Miss
Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate
Mwegelo, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo
cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea
kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni
mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti.Miss
Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate
Mwegelo, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo
cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea
kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni
mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na
Jumanne Juma.
No comments:
Post a Comment