Wakazi wa Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam, wakiwa katika foleni ya kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Kilimani, katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.Picha na Maktaba |
Akisoma matokeo hayo jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi
wa Tamisemi, Khalist Luanda alisema matokeo hayo yamekamilika kwa
asilimia 99 kutokana na baadhi ya maeneo kutofanya uchaguzi kutokana na
sababu mbalimbali ikiwamo wagombea kufungua kesi mahakamani na baadhi ya
wagombea kufariki dunia kabla ya uchaguzi.
Jumla ya vyama 15 vilishiriki uchaguzi huo
vikiwamo CCM, Chadema, CUF, NCCR - Mageuzi, TLP, NLD, ACT, UDP na APPT-
Maendeleo. Vingine ni Chauma, NRA, UMD na vitatu ambavyo havikuambulia
kiti hata kimoja vya DP, Tadea na ADC.
Matokeo
Pamoja na CCM kuendelea kuongoza kwa ujumla, chama
hicho kimeonekana kupoteza viti mijini na vijijini na kimeporomoka
zaidi mijini.
Katika maeneo ya vijiji na vitongoji, chama hicho
kimepata ushindi wa asilimia 79.81 (vijiji) na 79.83 katika vitongoji,
wakati kwenye mitaa ambayo ipo sehemu za mijini kimeshuka zaidi na
kupata asilimia 66.66.
Matokeo hayo yakilinganishwa na yale ya mwaka
1999, chama hicho kilipata asilimia 89.2 katika mitaa, asilimia 91
katika vitongoji na asilimia 91.6 katika vijiji.
Matokeo ya vijiji
Idadi ya vijiji vyote Tanzania Bara vilivyotarajiwa kufanya uchaguzi ni 12,443 lakini umefanyika katika vijiji 11,750.
Matokeo ya vyama pamoja na asilimia katika mabano
ni CCM 9,378 (79.8), Chadema 1,754 (14.9), CUF 516 (4.4), NCCR Mageuzi
67 (0.6) na TLP 10 (0.09). Vingine ni UDP 14, ACT 8 (0.07), NLD 2 (0.02), (0.12) na NRA 1 (0.0001).MWANANCHI
No comments:
Post a Comment