Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Picha na Exaudi Mtei. |
Na Mwandishi Wetu
WAKATI bado kukiwa na vuguvugu la kashfa ya Escrow, sanjari na wananchi kutafakari hatua alizozichukua Rais Dkt.Jakaya Kikwete kuhusiana na kashfa ya Escrow kwa ujumla wake pamoja na mapendekezo ya Bunge kuhusu ufisadi wa zaidi
sh. bilioni 200 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow,umoja wa vyama vya upinzani maarufu kama Ukawa umemjibu Rais.
Umoja huo umesema kuwa Rais anahusika kwa kiasi kikubwa
kwenye sakata hilo hasa kwa kitendo chake cha kumtetea mmiliki wa kampuni ya Indepent Power Solution Limited , IPTL Harbnder Singh.
Kutokana na kutoridhishwa na maamuzi hayo ya Rais Ukawa umeazimia kufanya maandamano
nchi nzima kupinga ufisadi huo ambao wanadai 'unalindwa' kiaina na Rais Kikwete.
Kauli hiyo ya Ukawa imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo wakati mkutano ulioitishwa na Ukawa,Prof.Lipumba pia ni Mwenyekiti wa CUF.
Profesa Lipumba aliongeza kusema inasikitisha
kuona Rais Kikwete ameacha kulitetea Shirika la Umeme Tanesco na
kuwatetea "matapeli" wa IPTL ambao wameliongizia shirika hilo hasara la mabilioni ya fedha
“Hutuba ya
Rais Kikwete imekuwa mtetezi mkubwa wa mmiliki wa PAP,anaacha kulitetea shirika
la umma na kusema kuwa pesa za
IPTL si za Umma hivi anashindwa hata kuielewa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali
CAG ambayo inaonyesha wazi kwamba
wamiliki hawa wamefanya 'utapeli'wa wazi kabisa katika umiliki wake? alihoji
Profesa Lipumba alidai hata maazimio yanayotokana na taarifa ya CAG yanaonyesha wazi kuwa PAP siyo mmiliki
wa halali wa hisa za Kampuni ya Mechmar lakini Rais Kikwete hakuliona hilo.
Pichani ni Dkt. Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa Chadema akizungumza katika mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam |
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Ukawa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa amesema Umoja huo umepanga kuzunguka nchi
nzima kufanya maandamano kupinga kile wanachodai Rais Jakaya Kikwete
kuwalinda mafisadi.
Dkt. Slaa aliongeza kuwa kitendo cha
Rais Kikwete kuwatetea wamiliki wa kampuni ya IPTL ni ishara kuwa Rais ana uhusiano na watuhumiwa hao.
James mbatia,Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi |
Naye Mwenyekiti NCCR Mageuzi
James Mbatia alidai kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Rais katika sakata hilo huku fedha za wananchi zikipotea na wabunge kutolipwa mishahara yao kwa wakati.
Umoja huo unaundwa na vyama vya
Vyama CHADEMA,CUF ,NCCR na NLD.
No comments:
Post a Comment