Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa
(kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi
na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida wakipitia
ratiba ya mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya
Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, mjini
Arusha
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(kushoto), Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati)
pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues wakishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na wafanyakazi wa
taasisi hiyo.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) akiteta jambo na Rais Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya pili ya Taasisi ya
Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni
mwa wiki Tengeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO
Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki. |
Rais
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika tete-a-tete na Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa
(UNESCO), Getachew Engida (kaitkati). Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa
shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA
la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema
linafanyakazi na nchi 20 za Afrika kutengeneza mifumo ya kitaifa ya
sayansi, teknolojia kusaidia mataifa hayo kufikia malengo yao ya
maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Getachew Engida
wakati alipopata nafasi ya kutoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali
ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia
iliyopo Tengeru mjini Arusha.
Alisema
shirika lake limejikita zaidi kuhakikisha kwamba inatoa elimu
itakayowezesha mabadiliko ya sayansi na hivyo kuwezesha wanaume kwa wake
kufanyakazi kama wajasirimali.
“Elimu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ukusanyaji takwimu, uimarishaji wa
viashiria na ubunifu wa vifaa vya ufuatiliaji na kuimarisha
utenegenezaji wa sera kwa kuangalia matukio yaliyothibitishwa,” alisema
Naibu Mkurugenzi huyo.
No comments:
Post a Comment