Aliyekuwa
Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh
amesema mihimili mitatu ya nchi ambayo ni Bunge, Mahakama na Serikali
isipofanya kazi bila kuangalia mipaka yao kwa mujibu wa sheria nchi
haitatawalika.
Amesema
utendaji wa siku kwa siku wa mihimili hiyo unatakiwa kupimwa kwenye
mizani ili kila mhimili ufanye kazi bila kuingilia kazi za mihimili
mingine kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kulinda amani ya nchi pia
kuongeza utawara bora na wenye maadili mema.(MM)
Utouh
ameyasema haya leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea tuzo ya
uadilifu na utawala bora kutoka kwenye kampuni ya Dream Success
Enterprises baada kuutambua umuhimu wa utendaji kazi wake akiwa kazini
kabla ya kustaafu.
Amesema
ubabe na kutoelewana huku kila mhimili ukitaka kujiona kuwa upo juu ya
muhimili mwingine kuna weza kukaleta machafuko makubwa yatakayoigharimu
nchi, na kwamba kurudisha amani itachukua muda.
"Kuna
haja ya hiii mihimili kufungiwa mizani, kufanya kazi kwa kutoingiliana,
pia ikiheshimiana na kutatua mambo yao kwa hekima Tanzania itakuwa
sehemu tulivu, yenye amani na kimbilio la wanyonge, lakini kama kila
muhimili ukifanya kazi kivyake bila kuzingatia sheria machafuko yanaweza
kutokea na kuifanya nchi isitawalike,"anasema Utouh.
Anasema
katika harakati zake akiwa kazini atalikumbuka daima sakata la uchotwaji
wa fedha katika akaunti ya nje (EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa
katibu Mkuu wa Nishati na Madini David Jairo.
Anasema
hayo yote yaliwezekana kufanyika kwa sababu mihimili ya Serikali ilikuwa
ikifanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu bila kuingiliana katika
maamuzi.
Anasema
tuzo aliyopata anaipokea ingawa katika kipindi chake cha kazi ndipo
kulipozaliwa jina la ufisadi, hata hivyo amesema anajivunia kuwepo kwake
katika ofisi ya CAG kwani alifanikwia kurudisha imani ya chombo hicho
kwa wananchi na hivi sasa wananchi wanakiamini
No comments:
Post a Comment