Waziri wa Fedha Saada Mkunya |
Wakati
Watanzania wakisubiri kwa hamu kujua iwapo wafadhili wa miradi ya
maendeleo wameridhishwa na hatua aliyoichukua Rais Jakaya Kikwete dhidi
ya kashfa ya kampuni ya IPTL ya uchotwaji wa mabilioni ya shilingi
katika akaunti ya Tegeta Escrow, ili waachie fedha walizozizuia kutokana
na suala hilo, serikali imeeleza kuwapo kwa matumaini yakiwamo ya
kuendelea kwa mazungumzo.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salim, alisema hayo jana alipozungumza kwa njia ya simu na NIPASHE.
Alisema wafadhili hao, ikiwamo Serikali ya Denmark, wamekuwa wakiendelea na majadiliano kuhusu msaada wao wa kifedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini hata kabla ya Rais Kikwete kuonyesha jitihada za kulivalia njuga suala la akaunti hiyo.
“Wameanza ‘kudiscuss’ (kujadili) hilo hata kabla ya Rais Kikwete kuchukua hatua hiyo. Kwa mfano, Denmark wameshaanza ‘kudiscuss’ (kujadili),” alisema Mkuya.
Alisema walichokuwa wanakisubiri wafadhili hao kilikuwa ni kutaka kuona hatua itakayochukuliwa na serikali, ikiwamo taarifa ya ukaguzi kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu kashfa hiyo. “Wao (wafadhili) ‘commission’ yao ilikuwa ni kuona hatua itakayochukuliwa na serikali na kuona CAG amefanya kazi yake na taarifa kutolewa,” alisema Mkuya. Juzi Serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake nchini, ililiambia gazeti hili kuwa shirika lake linaloshughulika na changamoto za milenia (MCC), ilikuwa inaisubiri serikali ya Tanzania kuonyesha hatua madhubuti za kushughulikia kashfa hiyo ili kuingizwa katika mkataba wa pili kwa ajili ya kupatiwa fedha za miradi ya maendeleo.
Katika mkutano huo wa kila mwaka uliofanyika Desemba 10, kwa ajili ya kujadili nchi zitakazoingizwa katika mkataba huo wa pili, MCC lilieleza kusikitishwa na taarifa za rushwa, likiwamo suala la akaunti hiyo.
Pia MCC ilieleza kuridhishwa na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati wa sherehe za uhuru kwamba, atashughulikia suala hilo na hivyo kusubiri kwa hamu hatua, ambazo alitarajia kufanya ili Tanzania ifikie maamuzi ya mwisho ya kuiingiza kwenye mkataba huo wa pili na kupewa fedha kwa ajili ya maendeleo. Kati ya mwaka 2008 na 2013 MCC walitekeleza mradi wa dola za Marekani milioni 698 katika sekta za maji, barabara na nishati nchini. Kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kwenye akaunti hiyo, ilisababisha baadhi ya wafadhili wa miradi ya maendeleo kusitisha misaada ya kifedha yenye thamani ya Sh. trilioni moja. Baadhi ya wafadhili hao, wakiwamo Denmark, Finland walieleza kuridhishwa na hatua iliyochukuliwa na Rais Kikwete ikiwa ni pamoja na kusubiri utekelezaji wa uchunguzi kwa watuhumiwa waliobaki.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment