Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Maria Alina Kimaryo (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa (kushoto) na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canicius Joseph wakizindua huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Wateja wa benki hiyo sasa wanaweza kupata huduma za kibenki kwa kutumia program maalum ya NBC katika ‘play store’ hivyo kupata huduma za kibenki kupitia laptop zao, tablets na simu za mkononi za smartphones. |
Mshauri
wa Bidhaa wa Benki ya NBC, Canisius Joseph (kulia), akionyesha jinsi huduma
mpya ya NBC Benki Nilipo inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma
hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina
Kimaryo, Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa na
Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe. |
Meneja wa
ATM na Kadi wa Benki ya NBC, Wambura John (katikati) akimwonyesha mmoja wa mteja,
Nusra John (kulia) jinsi anavyoweza kutoa pesa katika ATM ya benki hiyo bila ya
kuwa na kadi kwa kutumia huduma ya NBC Cash Popote katika hafla ya uzinduzi wa
huduma ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Huduma
za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter. |
Mkuu wa Kitengo
cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa (Kkushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo.
Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo na Mshauri wa Bidhaa
wa benki hiyo, Canisius Joseph.
|
Meneja Mahusino wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akiweka mambo sawa katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo. |
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC wakishuhudia uzinduzi wa NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. |
Baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini ar es Salaam leo. |
No comments:
Post a Comment