Na Pamela Mollel,Arusha
Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Arusha kimesema hakipingani na
makundi yoyote yanayokwenda kumshawishi Mbunge wa Monduli na Waziri
Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa kuchukua fomu ya kuwania urais katika
uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu na kusema
kuwa Sauti ya watu ni Sauti ya Mungu.
Aidha Umoja wa Vijana wa CCM(Uvccm) mkoani hapa kimedai kushangazwa
na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,ya kudai
kuwa kitendo cha makundi ya watu wanaokwenda nyumbani kwa Lowasa
kumshawishi agombee Urasi, hakumwondolei Lowasa sifa za kuwania urais
kwa kuwa hakuna kipengele kwenye Katiba au Kanuni ya CCM kinachokataza
wanacahama kufata viongozi.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM
mkoani hapa,Isaack Joseph alipokwua akizungumza na waandishi wa habari
katika makao makuu ya chama hicho na kusema kuwa kimeshangazwa na kauli
ya Nnauye kwani kinachofanyika ni utekelezaji wa kauli ya Rais Jakaya
Kikwete aliyoitoa katika sherehe za CCM mjini Songea alipowaruhusu watu
wakawashawishi wanaoona wanafaa kuwania urais.
Alisema kwamba kwa tabia na mila za kiafrika mtu akitembelewa na
mgeni hana budi kumkaribisha ,kumkirimu pamoja na kumfanyia maandalizi
yote na kusema kuwa makundi mbalimbali yameona Lowasa anafaa ndio
maana yamekwenda kumshawishi agombee.
“Kama kuna makundi yanayomfuata Lowasa na yaende kwani Sauti ya watu
ndio sauti ya Mungu watu wameona anafaa ndio maana wamemfuata
kumshawishi sasa kunamuondoleaje sifa?”alihoji JosephHatahivyo,alisema kuwa Lowasa tangu apewe adhabu ndani ya chama hicho
hakuwahi kuongea lolote na hata baada ya kufunguliwa adhabu hiyo baadhi
ya makundi yamekuwa yakimfuata kwa kuona anafaa na kumtaka Nnauye
kuacha kuropoka hovyo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha,Isaack Joseph akizungumza na waandishi wa habari jana katika makao makuu ya chama hicho na kudai kushangazwa na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye ya kuwa makundi yanayokwenda nyumbani kwa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, kumshawishi kugombea Urais kuwa na kusema kuwa makundi hayo yanachokifanya ni utekelezaji wa kauli ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika sherehe za CCM mjini Songea, alipowaruhusu watu wakawashawishi wanaoona wanafaa kuwania nafasi mbalimbali.(Habari Picha na http://jamiiblog.co.tz/ |
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM),Mkoa wa Arusha, Robinson Meitinyiku, akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa Habari, ambapo amekitaka Chama hicho kusimamia misingi, katiba na kanuni kwa wanachama na kukaripia wote wanaofanya makosa na kumtaka Nape kuheshimu na kutambua maadili ya utu na kumtaka atambue kuwa Lowasa ana watu nyuma yake ambao wanampenda, kumheshimu na kumjali, hivyo UVCCM hawatakaa kimya kuwasemea wanyonge wanaokwenda kumshawishi Lowasa agombee..hapo akifafanua Katiba ya CCM inavyowapa wanachama fursa ya kuwaona viongozi wao. |
Katibu Mwenezi akizungumza na waandishi wa habari jana, katika Makao Makuu ya Chama hicho. |
No comments:
Post a Comment