Ndege ya shirika la Germanwings, Airbus yenye namba A320 na namba ya
safari 4U 9525 iliyokuwa ikitoka Barcelona nchini Hispania kwenda
Duesseldorf nchini Ujerumani ilianguka kutoka angani mpaka chini ya
ardhi kwa muda wa dakika 8 umbali wa futi 38,000 katika milima ya Alps
iliyopo nchini Ufaransa.
Mkurugenzi wa shirika la ndege la Germanwings, Thomas Winkelmann
amesema wasafiri 72 kati ya 144 walikuwa raia wa Ujerumani. Wahanga
wengine walikuwa ni wanafunzi 16. Wakati huo nchi ya Hispania ikisema
watu 51 walikuwa ni raia wa nchini humo. Katibu wa UK Foreign, Philip
Hammond amehakikisha kuwa watu 3 walikuwa ni Waingereza.
wengine walikuwa ni kutoka nchi za Australia, Argentina, Iran,
Venezuela, Marekani, Uholanzi, Colombia, Mexico, Japan, Denmark na
Israel.
Uchunguzi wa awali wa sauti
zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka
Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa ndege hiyo alikuwa
amefungiwa nje ya eneo la marubani wakati ndege hiyo ilipoanguka.
Aidha haijabainika kikamilifu alikuwa ameondoka kufanya nini lakini
sauti zinasikika akibisha kwa nguvu akitaka ufunguliwe mlango.
Duru za kuaminika zinanukuliwa na jarida la New York Times.
Mkuu wa shirika la ndege la Lufthansa amesema kwa kinywa wazi kuwa kuanguka kwa ndege hiyo kuna hila hila.
''Hakuna maelezo kamili ya kiini cha ajali hiyo ''
''Ndege hiyo ilikuwa imefanyiwa ukarabati majuzi tu wala haikuwa na hitilafu yeyote''.
Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha
kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya
shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.
Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine
,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo .
Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa
Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa
katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.
David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege ,anasema kwamba
visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini kilichotokea.
Pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi wa ndege
hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo ambalo
walijaribu kulitatua pamoja kama timu, na hatua walizochukua kunusuru
janga hilo.
No comments:
Post a Comment