Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akimkabidhi cheti Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Magdalena Chuwa kwa kutambua
mchango wa taasisi katika kufanikisha kongamano la maadhimisho ya miaka
10 ya Tume ya Utumishi wa Umma.
Ndugu
msomaji, jana tulizungumzia tatizo la Lumbesa, hebu leo tuangalie ufumbuzi wake
kama anavyoeleza Afisa Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa.. endelea.
Kwa
mujibu wa Chuwa , Wakala umependekeza mikakati mbalimbali ambayo inaweza
kusaidia kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la ufungashaji batili wa bidhaa kwa
mtindo wa Lumbesa.
Mojawapo ya mikakati hiyo ni kuwepo kwa faini kubwa kwenye sheria mpya ya
vipimo ili iweze kuzuia ufungashaji huu batili wa ambao humsababishia mkulima
umasikini badala ya kumnufaisha .
Mkakati
mwingine ni utoaji wa elimu kwa umma katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu
hususan mikoa ya Iringa na Mbeya ambako kuna uzalishaji mkubwa wa mazao
mbalimbali.
“Hivi
sasa Wakala wa Vipimo umekuwa ukipata fursa ya kutoa elimu kwa njia ya mada
kuhusu majukumu yake,katika vikao vya RCC huko mikoani.Mada hizo husaidia
viongozi wa juu mikoani kufahamu kwa undani zaidi madhara ya vipimo batili kama
Lumbesa,Visado na Madebe kwa wafanyabiashara na wakulima,”
Chuwa
anasema kuwa licha ya kuendelea kutoa elimu kwa viongozi wa juu mikoani,pia
Wakala unaendelea na mkakati wa kuelimisha wananchi wa ngazi za chini kabisa
kwa msaada wa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa.
“Tunaimani
kuwa elimu ndiyo suluhisho la uhakika kwa changamoto za matumizi ya vipimo
batili nchini ambavyo husababisha wakulima na wajasiriamali kuendelea kuwa
masikini siku hadi siku” aliongeza Chuwa. ...Tutaendelea Jumatatu.
No comments:
Post a Comment