Chirstopher Mzazi katikaki akiwainua juu mabondia Julius Kisalawe kushoto na Said Uwezo kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumamosi ya march 28 utakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park ccm tandale Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Julius Kisalawe kutoka Ndame
Clab na Said Uwezo kutoka Mzazi GYM wamepima uzito kwa ajili ya mpambano
wao wa ubingwa wa taifa utakao fanyika katika ukumbi wa manyara park CCM Tandale March 28 Jumamosi
Mpambano huo utakuwa chini ya
oganaizesheni ya mchezo wa ngumi za kulipwa T.P.B.O ambapo msimamizi wa
upimaji uzito Ibrahimu Kamwe ambaye alitoa taaarifa kuwa bondia Uwezo alikuwa
kazidi uzito na kumfanya apewe muda wa kupunguza uzito kwa masaa matano
zaidi ili afikie lengo lake la kugombanmia ubingwa uho ambao
unashikiliwa na Kisalawe
Bondia huyo alipunguza uzito kwa muda unaotakiwa na kuruhusiwa kuwania ubingwa huo wa kg 52
Mbali na mpambano huo siku hiyo
kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kusindikiza mtanange huo ambapo
bondia kutoka Super D GYM iliyopo shule ya Uhuru Vicent Mbilinyi
atapambana na Yusuph Mkali mpambano wa raundi sita ambapo kiingilio
katika mpambano huo ni silingi. 5000 tu na wanawake ni bure kabisa
siku hiyo kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa watu na mali zao
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi ,DVD hizo zimeandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu na zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo, Rajabu Mhamila ‘Super
D’, ambaye alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa
ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
No comments:
Post a Comment