Na. Johary Kachwamba – MAELEZO, DODOMA
…………………………………..
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetangaza
ugunduzi wa gesi asilia katika Miamba ya Mchanga kwenye kisima
kinachochimbwa na Statoil cha Mdalasini-1 kwenye bahari kuu ya Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene
amebainisha hayo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma.
Baada ya kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Statoil, Nick Maden pamoja
na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
“ugunduzi huo wa gesi asilia wa futi za ujazo trilioni
1.0-1.8, unaongeza kiwango cha gesi asilia iliyopatikana kwenye kitalu
namba 2 kufikia futi za ujazo trilioni 22. Kisima cha Mdalasini -1
kimechimbwa katika urefu wa mita za maji ya bahari 2,296 kusini mwa
kitalu namba 2” alisema Mhe. Simbachawene.
“kuanzia mwanzo wa uchimbaji, Februari 2012, tumechimba
visima 13 na tumefanya ugunduzi katika visima 8 ikiwemo Mdalasini-1.
Bado tunaona uwezekano wa gesi zaidi katika eneo la Kitalu namba 2”
aliongezea Mhe. Simbachawene
Statoil ni Mkandalasi katika Leseni ya Utafutaji ya Kitalu
namba 2 kwa niaba ya TPDC na inayohisa ya asilimia 65% na mshirika wake
ExxonMobil and Production Tanzania Limited inazo hisa asilimia 35%.
Wakati wa uendeshaji baada ya Serikali kutoa Leseni ya
uzalishaji, TPDC kulingana na mkataba inaweza kushiriki katika
uendeshaji na uzalishaji kwa kutwaa asilimia 10% ya uwekezaji.
No comments:
Post a Comment