Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Mrisho Millao (kushoto) akihakiki namba ya simu anayooneshwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) wakati wa kuchezesha droo ya 45 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo, ambapo mshindi wa pili wa kitita cha shilingi milioni 100 alipatikana. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au Auto kwenda 15544. |
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
kuchezesha droo ya 45 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na
kampuni hiyo na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo, ambapo
mshindi wa pili wa kitita cha shilingi milioni 100
alipatikana. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay
au Auto kwenda
15544. Kushoto ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini,Mrisho Millao
Wateja
wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania wamehimizwa kujenga
utamaduni wa kuacha simu zao zikiwa hewani ili waweze kupata
mawasiliano kwa urahisi muda wowote na mahali popote
wanapokuwa.
Wito
huo ulitolewa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
wakati wa droo ya 45 ya Promosheni ya Jaymillions ambayo imemuwezesha
mmoja wa wateja wa kampuni hiyo kujishindia kitita
cha shilingi Milioni 100/- ingawa alipopigiwa simu na maofisa wa
kampuni hiyo mbele ya waandishi wa habari na Msimamizi wa Bodi ya
Michezo ya kubahatisha nchini Mrisho Millao simu ya mteja huyo ikawa
haipatikani.
“Tunaelewa
zipo sababu zisizoweza kuzuilika ambazo zinaweza kusababisha simu ya
mteja isiwe hewani lakini vilevile kuna baadhi ya wateja wana utamaduni
wa kuzima simu ambao unaweza ukasababisha
mteja akose mawasiliano ya muhimu kama mteja wetu huyu leo ambaye
tulitaka kumpa taarifa ya kujishindia kitita chake kupitia promosheni
yetu ya Jaymillions”.
Alisema
kwa mjibu wa taratibu za Bodi ya Michezo ya kubahatisha kwa namba hiyo
ya ushindi kutopatikana wataendelea kufanya jitihada za kumtafuta
mshindi kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia
matangazo kwenye vyombo vya habari na kuendelea kumpigia mara kwa mara
kwa muda wa wiki mbili kuona kama kuna wakati atakuwa hewani.
Promosheni
ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwezi Januari mwaka huu ambayo
itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja
na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa
kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na
hadi kufikia sasa wameishapatikana washindi wawili wa milioni
100/-(akiwemo mshindi wa leo),washindi wanne wa Milioni 10/-na washindi
38 wa Milioni 1/-
Nkurlu
pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions
katika kipindi hiki ambacho inakaribia kufika mwishoni ili wajishindie
kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba
15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba
15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.
|
No comments:
Post a Comment