Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu ambaye alikuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu utendaji wa Shirika hilo leo asubuhi. Waziri Lukuvi yuko katika ziara ya siku mbili kushuhudia utendaji wa Shirika hilo ambapo leo na kesho atatembelea baadhi ya miradi ya NHC iliyopo jijini Dar es Salaam na kisha baadaye kuzungumza na wafanyakazi wa NHC. |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na James Rhombo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NHC, wakati akikaribishwa Makao Makuu ya NHC. Kulia na Felix Maagi, Hamad Abdallah na Raymondo Mndolwa. |
Waziri Lukuvi akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio kuingia kwenye ofisi za makao makuu ya NHC leo. |
No comments:
Post a Comment