Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi tarehe 02, Aprili 2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake. |
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani) |
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) akisoma hotuba ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa kwanza kushoto). Katikati ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe |
No comments:
Post a Comment