Na Anitha Jonas-MAELEZO,Dodoma.
……………………………….
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne
Makinda ametoa ufafanuzi juu ya suala la Muswada binafsi wa Baraza la
Vijana uliyowasilishwa na Mhe.John Mnyika Mbunge wa Ubungo (CHADEMA)
hapo mwaka jana.
Mhe.Makinda alisema Ofisi yake inataratibu zinazofuatwa katika
uwasilishwaji wa Miswada bungeni na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Maendeleo ya Jamii ilifanya taratibu zake na kuiletea Ofisi yake taarifa
ya makubaliano ya Muswada wa Serikali ndiyo utako somwa Bungeni baada
ya kufuata taratibu zote muhimu.
“Ofisi yangu haifanyi maamuzi binafsi katika uwasilishwaji wa
Miswada Bungeni na zipo hatua mbalimbali Miswada inayopitia pamoja na
Kanuni za Bunge zinatoa muongozo katika utekelezaji wake na Kamati
huzingatia hayo na mwisho hutoa taarifa ya kuomba Muswada kusomwa ndani
ya Bunge,”alisema Mhe.Makinda.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii
Mhe.Said Mtanda (Mb) wa Mchinga CCM alisema Kamati ilipokea Miswada
miwili ya kuundwa kwa Baraza la Vijana ukiwemo wa Mhe.John Mnyika Mb wa
Ubungo CHADEMA na Muswada wa Serikali.
Baada ya hapo Kamati ilikaa Kikao tarehe 20-31 Oktoba 2014 na
kujadili Muswada huo ambapo pamoja na mambo mengine iliwaita wadau
mbalimbali ambao walitoa maoni yao na mapendekezo ya Kamati,Kamati
iliona Muswada huo haukuwa tayari na hivyo ulirudishwa katika Ofisi ya
Spika tarehe 06 Novemba,2014.
Aidha,Kamati ilipokea Muswada wa Serikali kuhusu hoja ya
kuanzishwa kwa Baraza la Vijana Tanzania Muswada na Kamati ilipata
nafasi ya kuujadili kwa kina,kupata maoni,ushauri na mapendekezo ya
wadau na hivyo badae kamati iliamua kuwa mtoa hoja Binafsi na Serikali
wakutane na na kushauriana kisha kupata muafaka wa Muswada upi uingie
ndani ya bunge.
“Kamati ilipata nafasi ya kujadili hoja zote mbili na kufanya
uamuzi wa kidemokrasia wa mashauriano na maridhiano juu ya muswada upi
uingie ndani ya Bunge.Aidha Kamati ilizingatia Kanuni ya 177 ya Kanuni
za Kudumu za Bunge,inayosema akidi ya Mkutano wowote wa Kamati ya kudumu
itakuwa theluthi moja ya wajumbe wote wa kamati,kwenye kikao hicho
kulikuwa na wajumbe 13 kati ya 22 wa kamati nzima na hivyo theluthi moja
ya wajumbe hao ni 7,wajumbe 9 walipiga kura ya Muswada wa Serikali
usomwe bungeni wajumbe wanne wa walikataka Muswada binafsi uswomwe
bungeni”,alisema Mhe.Mtanda.
Mwisho Kamati ilikubali kwa pamoja mambo yote ya msingi yaliyomo
kwenye Muswada binafsi yatumike kuboresha Muswada wa Serikali
utakaowasilishwa Bungeni.
No comments:
Post a Comment