Hali
ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai anayemaliza
muda wake, mh Freeman Aikae Mbowe, imeendelea kuimarika.
Akizungumza
na waandishi wa habari muda mfupi uliopita katika Hospitali ya taifa ya
Muhimbili, anakopatiwa matibabu, mh Mbowe, amesema anaendelea vizuri na
kwamba bado anaendelea kupumzika hospitalini hapo, kama alivyopangiwa
na madaktari wanaoangalia hali yake.
''Hali
yangu imeendelea kuimarika na kilichonipata jana kwa mujibu wa
uchunguzi wa madaktari ni uchovu wa muda mrefu, uliobainishwa kutokana
na shughuli za muda mrefu bila kupumzika katika shughuli zangu za
kisiasa'' amesema Mbowe.
Mh
Mbowe ameongeza kwamba, madaktari wamemtaka kuendelea kuwa chini ya
uangalizi wao mpaka hapo watakapo mruhusu kuendelea na shughuli zake za
kwawaida.
Mmoja
kati ya madaktari wanaoangalia afya ya mh Mbowe, Dr Tulizo
Sanga(daktari bingwa wa magonjwa ya moyo) ,amewaambia waandishi wa
habari hospitalini hapo kwamba, mh Mbowe alipokelewa jana akitokea
Hospitali ya Doctors Plaza ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam, kwa ajili
ya uangalizi na uchunguzi zaidi kutokana na kuugua ghafla wakati akiwa
katika msafara wa mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa.
Mh Mbowe amelazwa katika hospitali ya Muhimbili, kitengo cha moyo, baada ya kuugua ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.
Mpekuzi
No comments:
Post a Comment